Ticker

6/recent/ticker-posts

JE WAJUA KUWA MUNGU ALIUMBA MITI YA KUWAPONYA BINADAMU?


Karibu ndugu msomaji kwenye makala yangu katika makala hii nitaweza kuongelea mambo yafuatayo:-
Je ni sahihi kupuuza dawa za asili?
Je ni dhambi kutumia dawa za asili?
Je ni kweli kwamba Mungu aliumba miti ya kuponya binadamu?

1.Je ni sahihi kupuuza dawa za asili?

Katika maisha yetu sisi binadamu tumefikia hatua mbaya ya kupuuza tamaduni zetu na kufuata mambo ya kigeni yenye madhara ndio sababu kwa sasa kumekuwa na magonjwa ya kutisha,

 tunapuuza vitu vya asili na kutumia vitu vya kitaaramu vyenye sumu  na kemikali zenye madhara. Kipindi cha zamani babu zetu waliishi miaka mingi kwasababu walikuwa wakila vyakula vya asili hiyo ilifanya mili yao kuwa na kinga na nguvu za uishi miaka mingi.

Ukiangalia kipindi kile hakikuwa na zahanati vituo vya Afya wala hospitali yoyote lakini leo pamoja na kuwepo huduma hizi za afya maisha ya watu yamekuwa mafupi sababu ya haya yote ni kubadili mfumo wa maisha leo binadamu wamekuwa wajinga ata panya anawazidi akili.

Inawezekana ukajiuliza kuwa kwanini panya amewazidi binadamu akili naomba unifatilie uta elewa, kitu ninacho ongelea, hapa ni swala la ulaji hata siku moja uwezi kumkuta panya anakula nafaka iliyo kobolewa kwasababu unapo koboa nafaka unatoa viini lishe vyote na vilutubisho unabaki na wanga tu ambapo kazi ya wanga ni kuupa mwili nguvu mwili unakuwa na nguvu lakini hauja jengwa wala hauna ulinzi.

Leo binadamu msomi mwenye elimu ya juu anakula nafaka iliyo kobolewa ambayo haina msaada kwenye mwili wake sasa mtu kama huyo elimu yake imemsaidia nini? Ndio maana kizazi cha leo magonjwa ni mengi sana kwakuwa vyakula vinavyo liwa kwa sasa ni vile vya wanga na vile vya kujenga mwili lakini vya kulinda mwili usishambuliwe na magonjwa tumeviepuka.

Leo mtu akiumwa ukimshauli atumie mizizi ya mti flani anakwambia mimi sitaki mambo ya kishirikina leo mizizi magome na majani ya miti yamegeuzwa ni ushirikina hizi ni mbinu za shetani kuwafanya watu wapuuze vitu vya asili watumie vya kitaalamu ili wapate madhara waweze kuteketea.

2.Je ni dhambi kutumia dawa za asili?
Hakuna andiko hata moja linalo sema msitumie dawa za asili hizo ni mbinu za shetani kuwatumia baadhi ya wachungaji na baadhi ya madhehebu kuubili kwa watu kwamba kutumia miti poli kwajili ya tiba ni ushirikina lakina hawa waambii watu kuwa kutumia dawa za kitaaramu kuna madhara viongozi wa dini kama hawa wanawachimbia kabuli waumini wao.
Ndugu zangu tusidanganywe biblia hukataza kuwaendea waganga wachawi na wapiga bao lakini hukataza kuchanja chale kwenye miili yao, Mungu amekataza hivyo kwatuwa watu hao ni vibaraka wa shetani japo wanatumia miti iliyo ubwa na Mungu kutibia watu lakini wanafanya hivyo kwa utukufu wa Shetani.
Kwa ufupi Mungu anahitaji tumtumikie yaye na tufanye yote kwa utukufu wake tukiwaendea vibaraka wa shetani tutakuwa tumeacha kumtumainia yeye na tumeona yeye hana msaada kwetu lakini shetani ndie mwenye msaada, lakini ukiambiwa na mtu dawa au wewe unafahamu mti unao tibu ugonjwa na ukatumia kujitibu sio dhambi.
Ni vema hao wachungaji wanao wadanganya waumini wao hivyo waache maana kwa kufanya hivyo wanamsaidia shetani kazi au kama wana ushahidi wa maandiko wanaweza kuyaleta hapa waandike sehemu ya maoni kama hawana wanyamaze milele na watubu kwa dhambi waliyo fanya ya kudanganya watu, 
3.Je ni kweli kwamba Mungu aliumba miti ya kuponya binadamu?
Ninacho waomba ndugu wasomaji Twendeni edeni tupate kupona tunaanza na Mungu alipo muumba adamu na eva aliwapa mboga matunda na nafaka wavitumie kwa chakula. 
Mwanzo 1
11 Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo.
12 Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. 

Mwanzo 1
29 Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;
30 na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.

Bila shaka utakuwa uki jiuliza maswali kuwa walikuwa wakitibiwa kwa njia gani kwa sababu hakukuwa na hospitali jibu ni kwamba walitumia miti matunda na nafaka kama chakula na dawa kwao. 
Naleta baadhi ya maandiko yanayo onyesha dawa za asili zilikuwa zikitumiwa na watu kwenye biblia kwajili ya kutibu magonjwa na kupata msaada kwa mambo mbalimbali.
Mungu alivyo umba bustani ya edeni kulikuwa miti mingi na aina nyingi za matunda lakini leo nataka kuongelea miti miwili miti wa kwanza uliinta mti wa ujuzi wa mema na mabaya huu ulikuwa katikati ya bustani ya edeni na ndio mti ambao Adamu na Eva walikatazwa kula, mwanzo  Mti wa pili ni mti wa uzima 
Mwanzo 2
8 Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.
9 Bwana Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.

. huu ndio mti wa ajabu wenye uwezo wa kutibu magonjwa yote na hata watakatifu watakula matunda ya mti huo ili wasife milele 
Ufunuo wa Yohana 22
2 katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.

Musa alitumia mti kutibu maji yaliyo kuwa makali 
Kutoka 15
23 Walipofika mahali palipoitwa Mara hawakupata kuyanywa yale maji ya Mara, kwa kuwa yalikuwa machungu; kwa ajili ya hayo jina lake likaitwa Mara.
24 Ndipo watu wakamnung'unikia Musa, wakisema, Tunywe nini?
25 Naye akamlilia Bwana; Bwana akamwonyesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, akawaonja huko;

Elisha alitumia mti kuibua shoka iliyo zama 
2 Wafalme 6
5 Lakini mmojawapo alipokuwa katika kukata boriti, chuma cha shoka kikaanguka majini; akalia, akasema, Ole wangu! Bwana wangu, kwani kiliazimiwa kile.
6 Mtu wa Mungu akasema, Kilianguka wapi? Akamwonyesha mahali. Akakata kijiti, akakitupa pale pale, chuma kikaelea.
7 Akasema, Kiokote. Basi akanyosha mkono, akakitwaa.

Elisha atumia unga kuondoa ukali kwenye matango poli 
2 Wafalme 4
39 Na mmoja wao akaenda nje kondeni ili kuchuma mboga, akaona mtango-mwitu, akayachuma matango-mwitu, hata nguo yake ikawa imejaa, akaja akayapasua-pasua sufuriani; kwa maana hawakuyajua.
40 Basi wakawapakulia hao watu ili wale. Ikawa, walipokuwa katika kula chakula, wakapiga kelele, wakasema, Mauti imo sufuriani, Ee mtu wa Mungu. Wala hawakuweza kula.
41 Lakini yeye akasema, Leteni unga. Naye akautupa ndani ya sufuria; akasema, Wapakulie watu, ili wale. Wala hakikuwamo kitu kibaya sufuriani.

Yakobo alitumia mti kuzalisha mifugo kwa wingi 
Mwanzo 30
37 Yakobo akatwaa fito za mlubna mbichi, na mlozi, na mwaramoni, akazibambua maganda, mistari myeupe ionekane ndani ya hizo fito.
38 Akazisimamisha fito hizo alizozibambua katika mabirika ya kunyweshea maji, pale walipokuja wanyama wanywe; wakachukua mimba walipokuja kunywa.
39 Wanyama wakapata mimba mbele ya hizo fito, wakazaa wanyama walio na milia, na madoadoa, na marakaraka.
40 Na Yakobo akawatenga wana-kondoo, akazielekeza nyuso za makundi zielekee wale waliokuwa na milia, na kila aliyekuwa mweusi katika wanyama wa Labani. Akaweka kando wanyama wake mwenyewe, wala hakuwachanganya pamoja na wanyama wa Labani.

Namani aliponywa ukoma kupitia maji kwa imani.
2 Wafalme 5
14 Ndipo akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi.

Yesu nae aliponya kwa kutumia udongo mate na maji. 
Yohana 9
6 Alipokwisha kusema hayo, alitema mate chini, akafanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu tope za macho
7 akamwambia, Nenda kanawe katika birika ya Siloamu, (maana yake, Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi anaona.

Nimeorodhesha mafungu ya biblia hapo ili kuonyesha nguvu ya vitu vya asili katika kuponya na kusaidia matatizo na kufanikisha mambo yetu lakini tunatakiwa kutambua kuwa mponyaji mkuu ni Mungu hivyo Mungu ameweka nguvu ya uponyaji na kupitia mimea matunda na miti, kwakuwa shetani anatambua siri hii ameitumia kuteka watu.

Ndio maana Twende Edeni tumeamua kukusaidia kuku patia elimu itakayo kusaidia kutambua miti mbalimbali matibabu yake na jinsi ya kuandaa na kutumia lakini pia ukihitaji dawa yoyote tunayo kufundisha wasiliana nasi, cha kuzingatia Follow blog yetu ili uweze kupata kila somo linalo tolewa.

 Siku ya leo napenda kukugusia mti wa Muembe poli

huu ni mti unao ota polini kwa maana ndio asili yake ndio maana ukaitwa kwa jina la Embe poli huu mti majani yake yanafanana na Embe la kawaida lakini yenyewe ni membamba malefu, lakini unaweza panda hata nyumbani kwako kwa kuwa unambegu huu mti unatibu magonjwa mengi.

Kwanza unatibu chango la uzazi,hili ni tumbo linalo uma mwanamke anapo elekea kupata siku zake na baada ya kuzipata, tumbo la uzazi yaani tumbo linalo uma baada ya mwanamke kujifungua, kwa wanaume hutibu ngili au mshipa, na pia hutibu tumbo la kuhalisha na tumbo la kawaida cha kufanya unapaswa kupima babla ya kutumia ili kuwa na uwakika na ugonjwa,

 kinacho tumika ni magome ya mti,
MAANDALIZI chukua chemsha kwa tatizo la chango la uzazi tumbo la uzazi na ngili kunywa lobo lita kutwa mala tatu kabla ya kula kwa siku 7 kwa tatizo la tumbo la kuhalisha na la kawaida kunywa lobo lita kutwa mala 3 kwa siku 3 ukipata huo mti waweza kutumia kutibu magonjwa niliyo kutajia 

kama ukikosa na unahitaji waweza kuwasiliana nami kwa namba 0759416497 dawa hizi naziandaa na unazipata kwa bei ndogo kabisa hata ukiwa mbali nakwagizia hazichanganywi na kitu chochote kinacho zingatiwa ni kubangua magome ya mti ulio komaa baada ya kufanya hivyo nasaga na kukausha na kuziweka kwenye vifungashio vyake.

Ukiwa na maoni au ushauri swali au ukiwa unahitaji dawa usisite kutuandikia maoni yako au wasiliana nasi kwa Email:twendeedeni@gmail.com na namba zilizo kwenye blog yetu Asante karibu sana kwenye blog yetu ya Twende Edeni sambaza na kwa mwingine.

MWANDAAJI NI
MUSA MZOPOLA

Post a Comment

0 Comments